Yohana 17 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Yesu awaombea wanafunzi wake

1 ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.

31 Yoh 5:20; 1 The 1:9 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

4Yn 4:34 Mimi nimekutukuza duniani, nikiwa nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

5Yn 1:1; 17:24; Flp 2:6 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

6Yn 17:9; Mt 6:9 Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.

7Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako.

8Yn 16:30 Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nilitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

9Yn 6:37,44 Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;

10Yn 16:15; Lk 15:31 na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.

11 Yn 10:30; Mt 6:13 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

12Zab 41:9; 109:8; Yn 13:18; 6:39; 2 The 2:3 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi niliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

13Yn 15:11 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.

14Yn 15:19 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

152 The 3:3; 1 Yoh 5:18; Mt 6:13; Lk 22:32 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.

16Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

17Yn 6:63 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.

18Yn 20:21 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo niliwatuma hao ulimwenguni.

19Ebr 10:10 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.

20 Yn 17:9 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.

21Gal 3:28 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

22Mdo 4:32 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.

231 Kor 6:17; Gal 2:20 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.

24Yn 10:29; 12:26; Efe 1:4 Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.

25Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nilikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.

26Nami niliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help