Zaburi 93 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Ukuu wa enzi ya Mungu

1 Isa 52:7; Ufu 19:6; Ayu 40:10; Zab 104:1; Isa 59:17 BWANA ametamalaki, amejivika adhama,

BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme.

Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;

2 Mit 8:22 Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani;

Wewe ndiwe uliye tangu milele.

3Ee BWANA, mito imepaza,

Mito imepaza sauti zake,

Mito imepaza uvumi wake.

4 Zab 29:10 Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu,

Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo,

BWANA Aliye Juu ndiye mwenye ukuu.

5Shuhuda zako ni amini sana;

Utakatifu ndio uifaao nyumba yako,

Ee BWANA, milele na milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help