Wakolosai 3 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Maisha mapya katika Kristo

1 Zab 110:1; Kol 2:12 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi katika mkono wa kuume wa Mungu.

2Mt 6:33 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.

3Rum 6:2 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

41 Kor 15:43; Flp 1:21; Gal 2:20 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.

5 Rum 6:6; 8:13; Efe 4:19; 5:3,5 Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo vya kidunia, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;

6Efe 5:6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.

7Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo.

8Efe 4:25-31; 5:4 Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na masuto, na matusi vinywani mwenu.

9Efe 4:22 Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake;

10Mwa 1:26; Efe 4:24 mkivaa utu mpya, unaofanywa upya katika ufahamu kulingana na mfano wake yeye aliyeuumba.

11Gal 3:28 Hapo hapana Mgiriki wala Myahudi, kutahiriwa wala kutotahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala muungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote.

12 Efe 4:2,32; 5:2; 1 Pet 2:9 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,

13Efe 4:32; 5:2; Mt 6:14 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.

14Rum 13:8,10; Efe 4:3 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.

15Efe 4:4; Flp 4:7; 1 Kor 12:13,27 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.

16Efe 5:19-20 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

171 Kor 10:31; Efe 5:20 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.

Mawaidha kwa familia

18 Efe 5:22–6:9; 1 Pet 3:1 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.

19Efe 5:25; 1 Pet 3:7 Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.

20Efe 6:1 Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.

21Efe 6:4 Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

22Efe 6:5-8 Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.

23Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,

24mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Yesu Kristo.

25Kum 10:17; Rum 2:11; Efe 6:9 Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help