1 Zab 2:5 BWANA, ni nani atakayekaa
Katika hema yako?
Ni nani atakayeishi
Katika kilima chako kitakatifu?
2 Zab 84:11; Isa 33:15,16 Ni mtu aendaye kwa ukamilifu,
Na kutenda haki.
Asemaye kweli kwa moyo wake,
3Asiyesingizia kwa ulimi wake.
Wala kumtenda mwenziwe mabaya,
Wala kumsengenya jirani yake.
4 Yos 9:18-20 Anayedharau waovu Machoni pake,
Bali huwaheshimu wamchao BWANA
Aliyeapa ingawa kwa hasara yake,
Hayabadili maneno yake.
5 Eze 18:8,9 Asiyetoa fedha yake apate kula riba,
Asiyepokea rushwa amwangamize asiye na hatia.
Mtu atendaye mambo hayo
Hataondoshwa milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.