1 Kol 4:3; 1 The 5:25 Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa kote kama ilivyo kwenu;
2na tukaokolewe kutoka kwa watu wasio haki, na waovu, maana si wote walio na imani.
31 The 5:24 Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu.
41 The 4:10; Gal 5:10; 2 Kor 7:16 Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tuliyowaagiza na kwamba mtaendelea kuyafanya.
5Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na subira ya Kristo.
Onyo juu ya kutofanya kazi6 Mt 18:17; Rum 16:17; 1 The 5:14; 4:1 Ndugu, tunawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.
71 The 2:1; 1:6 Mnajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata; kwa sababu hatukuenda bila utaratibu kwenu;
81 Kor 4:12; Flp 3:17; 1 The 2:9 wala hatukula chakula kwa mtu yeyote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulifanya kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote.
9Mt 10:10; 1 Kor 4:16; 1 The 1:6,7 Si kwamba hatuna haki hiyo, ila kwa makusudi ya kuwapa mfano wa kuiga, mtufuate.
10Mwa 3:19; 1 The 3:4; 4:11 Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.
111 The 5:14 Maana tunasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.
121 The 4:11 Basi tunawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.
13Gal 6:9 Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema.
141 Kor 5:9,11 Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la barua hii, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari;
151 The 5:13,14 lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.
Salamu za mwisho na baraka16 1 The 5:23 Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.
17 1 Kor 16:21 Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila barua yangu, ndio mwandiko wangu.
18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.