1 na miti ya mjohoro,
6na mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri;
7 moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.
11Nawe ulifunike kwa dhahabu safi, ulifunike ndani na nje, nawe tia na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote.
12Nawe subu vikuku vinne vya dhahabu kwa ajili yake, na kuvitia katika miguu yake minne; vikuku viwili upande mmoja, na vikuku viwili upande wake wa pili.
13Nawe fanya miti mirefu ya mshita na kuifunika dhahabu.
14Nawe tia hiyo miti katika vile vikuku vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku.
15 cha dhahabu safi; urefu wake utakuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu.
18Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku.
19Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi yawe kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.
201 Fal 8:7; 1 Nya 28:18 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema.
21Kut 26:34; 40:20 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku.
22Kut 29:42; 30:6,36; Law 16:2; Hes 17:4; Eze 9:3; Yak 2:13; 1 Sam 4:4; 6:2; 2 Fal 19:15; Zab 80:1; 90:1; Isa 37:16 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.
Meza ya mikate iliyowekwa mbele ya Mungu23 Kut 37:10; 1 Fal 7:48; 2 Nya 4:8; Ebr 9:2 Nawe fanya meza ya mti wa mshita; urefu wake utakuwa dhiraa mbili, na upana wake dhiraa moja, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.
24Uifunike dhahabu safi, na kuifanyia ukingo wa dhahabu wa kuizunguka pande zote.
25Kisha ifanyie upapi wa kuizunguka pande zote, upana wake utakuwa nyanda nne, nawe uufanyie ule upapi ukingo wa urembo wa dhahabu wa kuuzunguka pande zote.
26Uifanyie vikuku vinne vya dhahabu, na kuvitia vile vikuku katika pembe zake nne, katika miguu yake minne.
27Vile vikuku na viwe karibu na ule upapi, ili viwe mahali pa kutilia ile miti, ya kuichukulia meza.
28Fanya ile miti ya mti wa mshita, na kuifunika dhahabu, kwamba ile meza ichukuliwe kwayo.
29Kut 37:16; Hes 4:7 Nawe fanya sahani zake, na miiko yake, na makopo yake, na vikombe vyake vya kumiminia; vifanye vyote vya dhahabu safi.
30Law 24:5-8 Nawe utaiweka mikate ya wonyesho juu ya meza mbele yangu daima.
Kinara cha taa31 Kut 37:17; 1 Fal 7:49; Zek 4:2; Ebr 9:2; Ufu 1:12; 4:5 Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, kitako chake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho;
32Hes 8:4; Kut 37:18,19 nacho kitakuwa na matawi sita yenye kutoka ubavuni mwake; matawi matatu ya kinara upande wake mmoja, na matawi matatu ya kinara upande wake wa pili
33vikombe vitatu vilivyotengenezwa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja; tovu na ua; na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua; vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara;
34na katika hicho kinara vikombe vinne vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, matovu yake, na maua yake;
35na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, kwa hayo matawi sita yatokayo katika kile kinara.
36Matovu yake na matawi yake yatakuwa ya kitu kimoja nacho; kiwe chote pia kazi moja ya kufua, ya dhahabu safi.
37Ufu 1:12; Kut 27:21; 30:8; Law 24:3,4; 2 Nya 13:11; Hes 8:2 Nawe zifanye taa zake saba; nao wataziwasha hizo taa zake, zitoe nuru mbele yake.
38Na makoleo yake, na visahani vyake, vyote vitakuwa vya dhahabu safi.
39Kitafanywa cha talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo hivi vyote.
40Mdo 7:44; Ebr 8:5; Kut 26:30; Hes 8:4; 1 Nya 28:11,19 Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, uliooneshwa mlimani.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.