Mithali 13 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

1 1 Sam 2:25; Mit 9:7,8 Mwana mwenye hekima husikiliza mausia ya babaye;

Bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.

2Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake;

Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri.

3 Zab 39:1 Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake;

Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.

4Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu;

Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.

5 Kol 3:9; Rum 12:9 Mwenye haki huchukia kusema uongo;

Bali mtu mbaya huwa karaha, hupatwa na aibu.

6 Mit 11:3 Haki humlinda yeye aliye mnyofu katika njia yake;

Bali ubaya humwangusha mwenye dhambi.

7Kuna mtu anayejitajirisha, lakini hana kitu;

Kuna anayejifanya kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.

8Fidia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake;

Bali mtu maskini hasikii ogofyo lolote.

9Nuru ya mwenye haki yang'aa sana;

Bali taa ya mtu mbaya itazimika.

10Kiburi huleta mashindano tu;

Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.

11 Mit 20:21 Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka;

Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.

12Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua.

Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.

13 2 Nya 36:16 Kila anayelidharau neno hujiletea uharibifu;

Bali yeye anayeiogopa amri atapewa thawabu.

14 Mit 16:22; 15:24; 2 Sam 22:6; Zab 116:3 Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima,

Ili kuepukana na tanzi za mauti.

15Ufahamu mwema huleta upendeleo;

Bali njia ya muasi huangamiza.

16 Mit 12:23 Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa;

Bali mpumbavu hueneza upumbavu.

17Mjumbe mbaya huanguka maovuni;

Bali mjumbe mwaminifu ni afya.

18 Mit 15:5 Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa;

Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa.

19Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu;

Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.

20Nenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima;

Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.

21 Zab 32:10 Uovu huwafuatia wenye dhambi;

Bali mwenye haki atalipwa mema.

22 Mhu 2:26 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi;

Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.

23 Mit 12:11 Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini;

Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma.

24 Mit 19:18; 22:15 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe;

Bali yeye ampendaye humrudi mapema.

25Mwenye haki hula akaishibisha nafsi yake;

Bali tumbo la mtu mbaya litaona njaa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help