1Samweli 12 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Samweli atoa hotuba ya kuaga

1 wake, nilitwaa ng'ombe wa nani? Au nilitwaa punda wa nani? Au ni nani niliyemdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi.

4Nao wakasema, Hukutudhulumu, wala hukutuonea, wala hukupokea kitu kwa mkono wa mtu awaye yote.

5 wake ni shahidi leo, ya kuwa hamkuona kitu mkononi mwangu. Nao wakasema, Yeye ni shahidi.

6Kut 6:26; Neh 9:9-14; Zab 77:19,20; Hos 12:13; Mik 6:4 Samweli akawaambia watu, Ni yeye BWANA aliyewaweka Musa na Haruni, yeye ndiye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri.

7Isa 1:18; 5:3; Mik 6:2,3; Amu 5:11 Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za BWANA, kwa kutaja matendo yote ya haki ya BWANA, aliyowatendea ninyi na baba zenu.

8 Kut 2:23 Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia BWANA, ndipo BWANA akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa.

9Amu 3:12; 4:2; 13:1 Lakini wakamsahau BWANA, Mungu wao, naye akawauza na kuwatia katika mikono ya Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori, na katika mikono ya Wafilisti, na katika mikono ya mfalme wa Moabu, nao wakapigana nao.

10Amu 10:10-15 Nao wakamlilia BWANA, wakasema, Tumefanya dhambi, kwa kuwa tumemwacha BWANA, na kuwatumikia Mabaali na Maashtorethi; lakini sasa tuokoe kutoka katika mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia wewe.

111 Sam 3:20; Amu 4:6; 7:1; 11:29 BWANA akawatuma Yerubaali, na Baraka, na Yeftha, na Samweli, akawaokoa ninyi kutoka katika mikono ya adui zenu pande zote, nanyi mkakaa salama.

121 Sam 8:7,19; 10:19; Amu 8:23; Mwa 17:7 Hata mlipomwona Nahashi, mfalme wa wana wa Amoni, amekuja kupigana nanyi, mliniambia, Sivyo, lakini mfalme atatutawala; ingawa BWANA, Mungu wenu, ni mfalme wenu.

13Hos 13:11 Basi sasa, mtazameni mfalme mliyemchagua na kumtaka; tazameni, BWANA ameweka mfalme juu yenu.

14Kum 6:13; 10:12; 13:4; Yos 24:14; Zab 81:13; Mhu 8:12; Isa 3:10 Kama mkimcha BWANA, na kumtumikia, na kuisikia sauti yake, msiiasi amri ya BWANA, tena kama ninyi, na mfalme anayewatawala, mkimfuata BWANA, Mungu wenu, vema!

15Law 26:14; Kum 28:15; Yos 24:20 Bali msipoisikia sauti ya BWANA, mkiiasi amri ya BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya baba zenu.

16Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu.

17Mit 26:1; Yos 10:12; 1 Sam 7:9; Yak 5:16; 1 Sam 8:7; Hos 13:10 Je! Leo si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, kwamba atume ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu mlioufanya machoni pa BWANA, ni mwingi sana, kwa kujitakia mfalme.

18Kut 14:31; Ezr 10:9 Basi Samweli akamwomba BWANA, naye BWANA akatuma ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa BWANA sana, na Samweli pia.

19Mwa 20:7; Kut 9:28; 10:17; Zab 78:34,35; Mdo 8:24; Yak 5:15; 1 Yoh 5:16 Watu wote wakamwambia Samweli, Tuombee watumishi wako kwa BWANA, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme.

20Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa mioyo yenu yote.

21Yer 16:19; Hab 2:18; 1 Kor 8:4 Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili,

22Zab 106:8; Yer 14:21; Mal 1:2; Mt 11:26; Yn 15:16 visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana BWANA hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.

231 Kor 9:16; Mdo 12:5; Rum 1:9; Kol 1:9; 2 Tim 1:3; 1 Fal 8:36; 2 Nya 6:27; Yer 6:16 Lakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka

24Ezr 9:13 Mcheni BWANA tu, mkamtumikie kwa kweli kwa mioyo yenu yote; maana, kumbukeni jinsi alivyowatendea mambo makuu.

25Yos 24:20; Kum 28:36 Lakini kama mkiendelea kutenda mabaya, mtaangamia, ninyi na mfalme wenu pia.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help