Mwanzo 26 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Isaka na Abimeleki

1 Mwa 12:10; 20:2 Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Abrahamu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari.

2Mwa 12:1; Zab 37:3 BWANA akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia.

3Mwa 22:16-18; 20:1; 28:15; Zab 39:12; Ebr 11:9; Mwa 12:2; 13:15; Zab 105:9 Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako.

4Zab 72:17 Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.

5Mwa 22:16 Kwa sababu Abrahamu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.

6Isaka akakaa katika Gerari.

7Mwa 12:13; 20:2; 24:16; Mit 29:25 Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni dada yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso.

8Ikawa alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani, akamwona Isaka anachezacheza na Rebeka mkewe.

9Abimeleki akamwita Isaka, akasema, Yakini huyu ni mkeo, mbona ulisema, Ni dada yangu huyu? Isaka akamwambia, Kwa sababu nilisema, Nisife kwa ajili yake.

10Mwa 20:9 Abimeleki akasema, Ni nini hii uliyotutendea? Labda mtu mmojawapo angalilala na mkeo bila kufikiri, nawe ungalitutia hatiani.

11Zab 105:15 Basi Abimeleki akawaamuru watu wote, akisema, Amgusaye mtu huyu au mkewe lazima atauawa.

12 Mt 13:8; Mk 4:8; Ayu 42:12; Mt 6:33 Mwaka huo Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, naye akapata mavuno mara mia zaidi. BWANA akambariki.

13Mit 10:22 Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana.

14Mwa 37:11; Mhu 4:4 Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng'ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu.

15Mwa 21:30 Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Abrahamu babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza udongo.

16Kut 1:9 Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi.

17Basi Isaka akatoka huko akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko.

18 Mwa 21:31 Isaka akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Abrahamu babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Abrahamu; naye akaviita majina kufuata majina aliyoviita babaye.

19Watumwa wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika.

20Mwa 21:25 Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye.

21Wakachimba kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna.

22Mwa 17:6; Kut 1:7 Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.

23Akapanda kutoka hapo mpaka Beer-sheba.

24 Mwa 15:1; 24:12; 26:3; Kut 3:6; Mdo 7:32; Rum 8:31 BWANA akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Abrahamu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubariki, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.

25Mwa 12:7; 13:18; Zab 116:17 Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA. Akapiga hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko.

26 Mwa 21:22 Ndipo Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi rafiki yake, na Fikoli, jemadari wa jeshi lake.

27Amu 11:7 Isaka akawauliza, Mbona mwanijia, nanyi mmenichukia, mkanifukuza kwenu?

28Mwa 21:22,23 Wakasema, Hakika tuliona ya kwamba BWANA alikuwa pamoja nawe; nasi tukasema, Na tuapiane, sisi na wewe, na kufanya mapatano nawe

29Mwa 24:31; Zab 115:15 ya kuwa hutatutenda mabaya, iwapo sisi hatukukugusa wewe, wala hatukukutendea ila mema, tukakuacha uende zako kwa amani; nawe sasa u mbarikiwa wa BWANA.

30Mwa 19:3 Basi akawafanyia karamu, nao wakala, wakanywa.

31Mwa 21:31 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaapiana wao kwa wao, kisha Isaka akawapa ruhusa, nao wakaenda zao kwa amani.

32Ikawa siku ileile, watumwa wa Isaka wakaja wakampasha habari za kile kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, Tumeona maji.

33Mwa 21:31 Naye akakiita jina lake Shiba; kwa hiyo jina la mji huo ni Beer-sheba, hata leo.

Esau na wake zake Wahiti

34 Mwa 36:2 Esau alipokuwa mwenye miaka arobaini, akamwoa Yudaithi, binti Beeri, Mhiti, na Basemathi, binti Eloni, Mhiti.

35Mwa 27:46; 28:1,8 Roho zao Isaka na Rebeka zikajaa uchungu kwa ajili yao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help