Wagalatia 5 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

1 Gal 4:5,31; Mdo 15:10 Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.

Asili ya uhuru wa Mkristo

2 2 Kor 10:1 Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidi neno.

3Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote.

4Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.

5Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani.

6Gal 6:15; 1 Kor 7:19 Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.

7Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli?

8Gal 1:6 Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi.

91 Kor 5:6 Chachu kidogo huchachua donge zima.

10Gal 1:7; 2 Kor 11:15 Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewasumbua atachukua hukumu yake, awaye yote.

111 Kor 1:23 Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Kwa kufanya hivyo kikwazo cha msalaba kimeondolewa!

12Zab 12:3 Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao!

13 1 Pet 2:16 Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.

14Law 19:18 Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.

15Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.

Kazi za kimwili

16Basi nasema, Nendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

17Rum 7:15-23; Yak 4:5; 1 Pet 2:11 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

18Rum 8:14 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.

191 Kor 6:9,10 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,

20ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi,

21Efe 5:5; Ufu 22:15 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Tunda la Roho

22 Efe 5:9 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

231 Tim 1:9 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

24Rum 6:6; Kol 3:5; 1 Pet 2:11 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.

25Rum 8:4 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

26Flp 2:3 Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help