Zaburi 80 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Sala ya kurejeshwa kwa IsraeliKwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Yungiyungi, Agano. Zaburi ya Asafu.

1 Kut 25:22; Kum 33:2; 1 Sam 4:4; Zab 89:1 Wewe uchungaye Israeli, usikie,

Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi;

Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.

2Mbele ya Efraimu, na Benyamini, na Manase,

Uziamshe nguvu zako,

Uje, utuokoe.

3 1 Fal 18:37 Ee Mungu, uturudishe,

Uangaze uso wako nasi tutaokoka.

4Ee BWANA, Mungu wa majeshi, hadi lini

Utayaghadhibikia maombi ya watu wako?

5Umewalisha mkate wa machozi,

Umewanywesha machozi kwa kipimo kikuu.

6Unatufanya sababu ya ugomvi kwa jirani zetu,

Na adui zetu wanacheka wao kwa wao.

7Ee Mungu wa majeshi, uturudishe,

Uangaze uso wako nasi tutaokoka.

8 Isa 5:1,7; Yer 2:21; Eze 15:6 Ulileta mzabibu kutoka Misri,

Ukawafukuza mataifa ukaupanda.

9Ulitengeneza nafasi mbele yake,

Nao ukatia mizizi sana ukaijaza nchi.

10Milima ilifunikwa kwa kivuli chake,

Matawi yake ni kama mierezi ya Mungu.

11 Kut 23:31; Zab 72:8 Nao uliyaeneza matawi yake hadi baharini,

Na vichipukizi vyake hadi kunako Mto.

12 Isa 5:5 Kwa nini umezibomoa kuta zake,

Wakauchuma wote wapitao njiani?

13Nguruwe wa msituni wanauharibu,

Na hayawani wa kondeni wanautafuna.

14 Zek 1:12,16,17; Isa 63:15 Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi,

Utazame toka juu uone, uujie mzabibu huu.

15 Isa 49:5 Na mche ule ulioupanda

Kwa mkono wako wa kulia;

Na tawi lile ulilolifanya

Kuwa imara kwa nafsi yako.

16Umechomwa moto; umekatwa;

Kwa lawama ya uso wako wanapotea.

17 Zab 89:21; Kut 4:22; Zab 110:1; Dan 7:13,14; Yn 5:21-27 Mkono wako na uwe juu yake

Mtu aliye katika mkono wako wa kulia;

Juu ya mwanadamu uliyemfanya kuwa imara,

Kwa nafsi yako;

18Kisha hatutakuacha kwa kurudi nyuma;

Utuhuishe nasi tutaliitia jina lako.

19 Hes 6:25; Zab 27:4,9 Ee BWANA, Mungu wa majeshi, uturudishe,

Uangaze uso wako nasi tutaokoka.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help