1 Kut 13:21-22; 14:22-29 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
2wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
3Kut 16:4,35; Kum 8:3 wote wakala chakula kile kile cha roho;
4Kut 17:6; Hes 20:11 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
5Hes 14:16,23,29-30 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
6Hes 11:4,34 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.
7Kut 32:6 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.
8Hes 25:1-18 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu elfu ishirini na tatu.
9Hes 21:5-6 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka.
10Hes 16:41-49; 14:2,36; Ebr 3:11,17 Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakauawa na mharabu.
111 Pet 4:7 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiwa na miisho ya nyakati.
12Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.
13Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili.
14 1 Yoh 5:21 Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.
15Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo.
16Mt 26:26-28; Mk 14:22-24; Lk 22:19-20; Mdo 2:42 Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
171 Kor 12:27; Rum 12:5 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
18Law 7:6,15 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu?
191 Kor 8:4 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?
20Kum 32:17; Law 17:7; Zab 106:37; Ufu 9:20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.
212 Kor 6:15,16; Mal 1:7,12 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.
22Kum 32:21 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?
Fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu23 1 Kor 6:12 Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.
24Rum 15:2 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake.
251 Kor 14:2-10,22 Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuulizauliza, kwa ajili ya dhamiri;
26Zab 24:1 maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.
27Lk 10:8 Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuulizauliza, kwa ajili ya dhamiri.
281 Kor 8:7 Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyewaambia, na kwa ajili ya dhamiri.
29Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?
301 Tim 4:4 Ikiwa mimi natumia sehemu yangu kwa shukrani, kwa nini nitukanwe, kwa ajili ya kitu nikishukuriacho?
31Kol 3:17 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
32Rum 14:13 Msiwakoseshe Wayahudi wala Wagiriki wala kanisa la Mungu,
331 Kor 9:20-22 vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.