Yuda Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziMwandishi wa waraka huu ni Yuda, aliyekuwa nduguye Yesu na Yakobo, yule aliyekuwa msimamizi wa Baraza la Yerusalemu, na mwandishi wa waraka wa Yakobo.Muktadha wa waraka huu na yale yaliyomo kwenye waraka wa 2 Petro yanaashiria kuwa Yuda alikuwa amehamasishwa na ujumbe wa Petro. Yuda anaonesha kuwa alikusudia kuandika kuhusu wokovu, lakini akabadili nasaha zake ili kukemea mtazamo wa watu fulani wenye tabia mbaya, waliokuwa wakizunguka miongoni mwa waumini wakipotosha neema ya Mwenyezi Mungu.MwandishiYuda, ndugu yake Isa.KusudiKukumbusha waumini umuhimu wa kuitetea imani, na kuwaonya kuhusu watu waovu wanaozunguka miongoni mwao wakipotosha imani.MahaliHapajulikani.TareheMnamo 65 B.K.Wahusika WakuuYuda, Yakobo, na Isa.Wazo KuuYuda anasisitiza umuhimu wa kuitetea imani. Wapotovu na wazushi ni lazima waoneshwe wazi kwamba sio wa kweli. Yuda anaonya kwamba hukumu ya Mwenyezi Mungu itawafikia wale waliopotoka katika imani, kama vile ilivyowafikia Kaini, Kora, na Balaamu.Mambo MuhimuKuweka wazi walimu wa uongo na kuwakemea vikali. Anamalizia ujumbe wake kwa kuonesha wazi kwamba Mwenyezi Mungu anaweza kumlinda muumini, ili aweze kuishi maisha yaliyonyooka, na hatimaye kufika mbele ya Mwenyezi Mungu bila lawama wala mawaa.YaliyomoSalamu na utangulizi (1-4)Hukumu kwa walimu wa uongo (5-16)Adibisho na hitimisho (17-25).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help