1Ee Mungu uniokoe kwa jina lako,
unifanyie hukumu kwa uwezo wako.
2Ee Mungu, sikia maombi yangu,
usikilize maneno ya kinywa changu.
3Wageni wananishambulia,
watu wakatili wanayatafuta maisha yangu,
watu wasiomjali Mungu.
4Hakika Mungu ni msaada wangu,
Bwana ndiye anayenitegemeza.
5Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia,
kwa uaminifu wako uwaangamize.
6Nitakutolea dhabihu za hiari;
Ee Mwenyezi Mungu, nitalisifu jina lako
kwa kuwa ni vyema.
7Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote,
na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.