Ayubu 26 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Hotuba ya tisa ya AyubuAyubu anajibu: Utukufu wa Mwenyezi Mungu hauchunguziki

1Kisha Ayubu akajibu:

2“Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo!

Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu!

3Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima?

Nayo ni busara gani kubwa uliyoonesha!

4Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo?

Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?

5“Wafu wako katika maumivu makuu,

wale walio chini ya maji,

na wale wanaoishi ndani yake.

6Mauti iko wazi mbele za Mungu;

Uharibifu haukufunikwa.

7Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu;

naye huining’iniza dunia mahali pasipo na kitu.

8Huyafungia maji kwenye mawingu yake,

hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.

9Huufunika uso wa mwezi mpevu,

akitandaza mawingu juu yake.

10Amechora mstari wa upeo juu ya maji,

ameweka mpaka wa nuru na giza.

11Nguzo za mbingu nazo zatetemeka,

zinatishika anapozikemea.

12Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari;

kwa hekima yake alimkata Rahabu vipande vipande.

13Aliisafisha anga kwa pumzi yake;

kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.

14Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake;

tazama jinsi ulivyo mdogo mnong’ono tunaousikia kumhusu!

Ni nani basi awezaye kuelewa

ngurumo za nguvu zake?”

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help