Walawi Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziKitabu cha Walawi kinajulikana kama “Kitabu cha Makuhani,” jina lililotokana na tafsiri ya Maandiko Matakatifu kwa Kiyunani. Walawi walichaguliwa na Mwenyezi Mungu kuwa makuhani. Kitabu cha Walawi kina amri nyingi walizopaswa kuzitii na kuzitenda. Kazi ya ukuhani ilikuwa ya kushughulikia matatizo ya kila siku kuhusu uadilifu wa Waisraeli wote, jinsi ya kumwabudu Mwenyezi Mungu, na kuishi katika utakatifu kama watu wateule wa Mwenyezi Mungu.Katika Maandiko Matakatifu, Mwenyezi Mungu aliamuru kutolewa kwa sadaka na dhabihu, nazo zikapata maana kutokana na uhusiano wa agano la Mwenyezi Mungu na Israeli. Makusanyiko matakatifu yaliyofanyika katika mwaka yalitoa mwito kwa Waisraeli kufanya upya tabia na ile hali ya kutambua wajibu wao kama watu waliochaguliwa na Mwenyezi Mungu. Ondoleo la dhambi lilifanyika kupitia kumwaga damu wakati wanyama walipokuwa wanatolewa dhabihu, kufuatana na maelekezo yaliyokuwa yametolewa kupitia kwa Musa.MwandishiMusa.KusudiKuonesha kwa undani sheria zilizowaongoza Waisraeli, yaani makuhani pamoja na watu, katika agano la uhusiano na Mwenyezi Mungu.MahaliChini ya Mlima Sinai, wakati wa safari ya Waisraeli.TareheMnamo 1450–1410 K.K.Wahusika WakuuWalawi, Musa, Haruni (na wanawe Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari), na Walawi wote.Wazo KuuKitabu hiki cha tatu miongoni mwa Vitabu Vitano vya Musa, kimsingi kinashughulikia jinsi ya kuishi maisha matakatifu na kumwabudu Mwenyezi Mungu.Mambo MuhimuUtakatifu umetajwa mara nyingi katika kitabu hiki kuliko kitabu kingine chochote cha Maandiko Matakatifu. Mwenyezi Mungu anawafundisha Waisraeli jinsi ya kuishi maisha matakatifu: Mwenyezi Mungu mtakatifu, ukuhani mtakatifu, watu watakatifu, dhabihu takatifu, vyombo vitakatifu, vyakula vitakatifu, pamoja na sheria ya utakatifu kwa ajili ya maisha ya utaua.YaliyomoAmri na maelekezo ya kutoa dhabihu na sadaka (1:1–7:38)Haruni na wanawe wateuliwa na Mwenyezi Mungu kuwa makuhani (8:1–10:20)Sheria zinazosimamia usafi na unajisi (11:1–15:33)Siku ya Upatanisho (16:1-34)Sheria za utakatifu kimatendo (17:1–22:33)Sikukuu zilizoamriwa, na mambo mengine (23:1–24:23)Miaka maalum (25:1-55)Mambo ya kufanya ili kustahili baraka za Mwenyezi Mungu (26:1–27:34).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help