2 Wathesalonike Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziWaraka huu uliandikwa miezi michache tu baada ya ule wa kwanza. Baadhi ya watu walikuwa wamemwelewa vibaya Paulo, au waraka mwingine wa bandia uliosemekana kuwa ulitoka kwa Paulo ulikuwa umewafadhaisha Wathesalonike kuhusu kurudi kwa Isa. Paulo aliandika waraka huu ili kuwakumbusha yale aliyokuwa ametangulia kuwafundisha, akiwahakikishia waumini kuwa Al-Masihi atarudi kuwafariji waliomwamini na kuwaadhibu wale waliokuwa wakiwatesa. Aliwaambia kwamba siku ya Mwenyezi Mungu, yaani siku ya hukumu, haingewafikia mara moja, bali ingetanguliwa na matukio mbalimbali. Wakifahamu kuwa hakika Al-Masihi angerudi, iliwapasa waumini kuishi maisha matakatifu yasiyo na lawama.MwandishiMtume Paulo.KusudiKuondoa mkanganyiko kuhusu kuja kwa Isa Al-Masihi mara ya pili.MahaliKorintho.TareheMnamo 51–52 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Silvano na Timotheo.Wazo KuuKuwafariji Wathesalonike kwa ajili ya mateso, na kuwahimiza waishi maisha ya kumtukuza Mwenyezi Mungu.Mambo MuhimuKurudi kwa Isa Al-Masihi, na kuwaonya waumini wasiache kufanya kazi.YaliyomoFaraja kutokana na kurudi kwa Al-Masihi (1:1-12)Matukio kabla ya kuja kwa siku ya Mwenyezi Mungu (2:1–3:5)Mausia ya wafuasi wa Al-Masihi, na kuwatakia heri (3:6-18).