Zaburi 87 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 87Sifa za YerusalemuZaburi ya wana wa Kora. Wimbo.

1Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;

2Mwenyezi Mungu anayapenda malango ya Sayuni

kuliko makao yote ya Yakobo.

3Mambo matukufu yanasemwa juu yako,

ee mji wa Mungu:

4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli

miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:

Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,

nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,

“Huyu na yule walizaliwa humo,

naye Aliye Juu Sana mwenyewe

atamwimarisha.”

6Mwenyezi Mungu ataandika katika orodha ya mataifa:

“Huyu alizaliwa Sayuni.”

7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,

“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help