Nehemia Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziVitabu vya Ezra na Nehemia vinaenda sambamba na vitabu vya Mambo ya Nyakati, vikisimulia habari zinazofuata matukio ya Mambo ya Nyakati. Kitabu cha Nehemia kimepewa jina la mhusika wake mkuu ambaye ni Nehemia. Katika andiko la Kiebrania, kitabu hiki ni sehemu ya kitabu cha Ezra. Inaaminika kwamba nabii Malaki alikuwa akihudumu katika kipindi hiki.MwandishiInasadikika kwamba Nehemia au Ezra, au wote wawili waliandika kitabu hiki, kwa sababu mwanzoni Ezra na Nehemia vilikuwa kitabu kimoja.KusudiHabari za kurudi kwa Wayahudi kutoka uhamishoni, na kujengwa kwa ukuta wa Yerusalemu.MahaliYerusalemu.TarehePengine mnamo 445–432 K.K.Wahusika WakuuNehemia, Ezra, Tobia na Sanbalati.Wazo KuuKitabu hiki kinaonesha kutimizwa kwa unabii wa Zekaria na Danieli kuhusu kujengwa upya kuta za Yerusalemu.Mambo MuhimuKujengwa kwa ukuta wa Yerusalemu, na kurejeshwa kwa utaratibu wa ibada.YaliyomoNehemia anazijenga kuta za Yerusalemu, watu waliorudi (1:1–7:73)Marekebisho chini ya Ezra na Nehemia (7:73–13:31).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help