Warumi Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziPaulo aliwaandikia watakatifu huko Rumi waraka huu. Wengi wa waumini wa kundi hili walikuwa ni watu wa Mataifa. Paulo anaanza kwa kueleza kwamba wanadamu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo Wayahudi na watu wa Mataifa hawawezi kudai haki mbele za Mwenyezi Mungu, kwa sababu dhambi zao zinafuta haki hiyo. Lakini Mwenyezi Mungu, kwa neema yake, anatuhesabia haki tuliyoipoteza kwa dhambi, haki tunayoipata kupitia kwa kumwamini Mwanawe, Isa Al-Masihi. Kwa njia hii ya kuhesabiwa haki na Mwenyezi Mungu katika Mwanawe, tunaweza kuwa washindi katika maisha ya wafuasi wa Al-Masihi. Kisha Paulo anaeleza nafasi ya Wayahudi katika mpango wa Mwenyezi Mungu. Anamalizia waraka wake kwa kutoa maonyo kadha wa kadha kuhusu maadili.MwandishiMtume Paulo.KusudiPaulo kujitambulisha kwa kundi la waumini la Rumi kwa ajili ya maandalizi ya safari yake, na pia ili kueleza kwa muhtasari msingi wa mafundisho yake.MahaliKorintho.TareheMnamo 57 B.K.Wahusika WakuuMtume Paulo, na waumini wa Rumi.Wazo KuuMpango wa Mwenyezi Mungu wa wokovu na haki kwa wanadamu, kwa Wayahudi na pia watu wa Mataifa, kwa kuwa wote ni wenye dhambi (1:16-17).Mambo MuhimuUfunuo kuhusu adhabu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya dhambi, na haki ipatikanayo kupitia kwa imani kama msingi wa kuhesabiwa haki.YaliyomoUtangulizi (1:1-17)Watu wote hawana haki (1:18–3:20)Haki ipatikanayo kwa kumwamini Al-Masihi (3:21–5:21)Kushinda dhambi kwa uwezo wa Al-Masihi (6:1–8:39)Mpango wa Mwenyezi Mungu kwa Israeli (9:1–11:36)Misingi ya maisha ya wafuasi wa Al-Masihi (12:1–15:13)Mipango ya Paulo na mawaidha ya mwisho (15:14–16:27).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help