2 Nyakati Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziKitabu cha 2 Mambo ya Nyakati kinaendelea kuelezea historia ya Yuda. Sura za 1–9 zinaelezea kujengwa kwa Hekalu wakati wa utawala wa Mfalme Sulemani. Sura za 10–36 zinaelezea historia ya Ufalme wa Yuda hadi kufikia kuharibiwa kwa Yerusalemu na watu kupelekwa uhamishoni Babeli. Kitabu hiki kinazungumzia jinsi uhusiano wa watu na Mwenyezi Mungu ni jambo la muhimu kuliko vitu vyote. Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati kinaambatana na vitabu vya 1 na 2 Wafalme, kikitoa ufafanuzi wake. Ufalme wa Kaskazini, yaani Israeli, haujatajwa kabisa katika historia ya kitabu hiki.MwandishiMapokeo ya Kiyahudi husema ni Ezra.KusudiKuliunganisha taifa katika ibada ya Mungu wa kweli kwa kuonesha viwango vyake katika kuwahukumu wafalme. Habari za wafalme wenye haki wa Yuda, dhambi za wafalme waovu, na wapinzani wao wa kidini nyakati za utawala wao zimewekwa wazi.MahaliYerusalemu, na katika Hekalu.TareheKama mwaka wa 430 K.K.Wahusika WakuuSulemani, Malkia wa Sheba, Rehoboamu, Asa, Yehoshafati, Yehoramu, Yoashi, Uzia, Ahazi, Hezekia, Manase na Yosia.Wazo KuuKitabu hiki kinaonesha mpango wa Mwenyezi Mungu kwa Israeli. Pia kinaonesha kwa nini ufalme wa Daudi haukuruhusiwa kuendelea kwa muda mrefu. Kitabu hiki, kama kile cha kwanza, kinaonesha wajibu wa Mwenyezi Mungu katika historia ya watu wake na mwingiliano kati ya maisha ya kiroho na ya kisiasa. Wafalme wanapimwa kwa jinsi walivyokuwa waaminifu kwa Mwenyezi Mungu.Mambo MuhimuUtawala wa Sulemani, kujengwa kwa Hekalu, kuasi kwa makabila kumi, habari za wafalme wa Yuda, na kuharibiwa kwa ufalme wa Yuda na Wababeli mwaka wa 586 K.K.YaliyomoUtawala wa Sulemani (1:1–9:31)Wafalme wa Yuda (10:1–36:14)Kuanguka kwa Yerusalemu (36:15-23).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help