Maombolezo Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziJina la kitabu hiki ni “Ekah” kwa Kiebrania, maana yake “Jinsi gani”. Maombolezo ni wimbo wa maziko wa kuomboleza Yerusalemu na kuharibiwa kwa Hekalu. Nchi iliachwa bila mfalme, na watu walikuwa wamepelekwa utumwani. Mwenyezi Mungu alikuwa amewaonya kuwa wangeenda utumwani wakimwacha.Yeremia aliandika maombolezo haya kuonesha huzuni yake kubwa na kuumia moyoni kwa sababu ya uharibifu wa kutisha wa Yerusalemu. Maafa haya yalihusisha anguko la kuaibisha la utawala wa ukoo wa Daudi, kuangamizwa kabisa kwa kuta za mji, Hekalu, jumba la mfalme, na mji wote. Mwishowe walipelekwa uhamishoni Babeli.MwandishiMapokeo na maandishi ya Kiyahudi na ya Kikristo husema ni Yeremia.KusudiKuwafundisha watu kwamba kutomtii Mwenyezi Mungu huleta maangamizi.MahaliYerusalemu.TareheMnamo 586–585 K.K.Wahusika WakuuYeremia, na watu wa Yerusalemu.Wazo KuuKutafakari mateso na matumaini kwa Mwenyezi Mungu.Mambo MuhimuYeremia auomboleza mji wa Yerusalemu, Mwenyezi Mungu kugadhibishwa na dhambi, na hali ya kuwa na tumaini katika mateso.YaliyomoKuangamizwa kabisa kwa Yerusalemu (1:1-22)Hasira ya Mwenyezi Mungu, na kutafuta faraja (2:1-22)Kutafakari mateso, na kuweka matumaini kwa Mwenyezi Mungu (3:1-66)Utukufu wa awali wa Yerusalemu, na hali ya sasa ya ukiwa (4:1-22)Kumwomba Mwenyezi Mungu aoneshe huruma (5:1-22).