1Mwenyezi Mungu tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka;
waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu.
2Kila mmoja humwambia jirani yake uongo;
midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.
3Mwenyezi Mungu na akatilie mbali midomo yote ya hila
na kila ulimi uliojaa majivuno,
4ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda;
midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”
5“Kwa sababu wanyonge wanaonewa,
na wahitaji wanalia kwa uchungu,
nitainuka sasa,” asema Mwenyezi Mungu.
“Nitawalinda kutokana na wale
wenye nia mbaya juu yao.”
6Maneno ya Mwenyezi Mungu ni safi,
kama fedha iliyosafishwa katika tanuru,
iliyosafishwa mara saba.
7Ee Mwenyezi Mungu, utatuweka salama
na kutulinda na kizazi hiki milele.
8Watu waovu huenda wakiringa kila mahali
wakati yule aliye mbaya sana
ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.