Zaburi 131 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 131Kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevuWimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1Moyo wangu hauna kiburi, Ee Mwenyezi Mungu,

macho yangu hayajivuni;

sijishughulishi na mambo makuu kunizidi

wala mambo ya ajabu mno kwangu.

2Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu;

kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake,

kama mtoto aliyeachishwa kunyonya

ndivyo ilivyo nafsi iliyo ndani yangu.

3Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungu

tangu sasa na hata milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help