Wakolosai Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziNyaraka za Waefeso na Wakolosai zinaitwa pacha kwa sababu mambo yaliyomo yanafanana. Timotheo alishirikiana na Paulo huko Rumi katika kuandika nyaraka hizi mbili; Wakolosai ni mojawapo ya nyaraka za gerezani. Tikiko ndiye aliupeleka waraka huu Kolosai.Mji wa Kolosai ulikuwa umejengwa kama kilomita 160 kutoka Efeso kwenye Bonde la Lika, karibu na Hierapoli na Laodikia. Kwa kadiri ionekanavyo, Paulo alikuwa hajautembelea mji wa Kolosai, ila mji huu ulihubiriwa Injili na Epafra wakati Paulo alikuwa Efeso. Paulo alipata kuwafahamu waumini hawa akiwa Efeso katika safari yake ya pili kueneza Injili. Sasa alikuwa na wasiwasi kwa sababu alisikia kuwa mafundisho ya Unostiki yalikuwa yameingia katika kundi hilo la waumini. Mafundisho haya yalikuwa yakiuelekeza ujumbe wa Injili hatarini.MwandishiMtume Paulo.KusudiKupinga mafundisho ya uzushi katika kundi hilo la waumini, na kuwaonesha waumini kwamba wana kila kitu wanachokihitaji katika Al-Masihi.MahaliRumi.TareheMnamo 60 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Timotheo, Tikiko, Onesimo, Aristarko, Marko, na Epafra.Wazo KuuKuthibitisha utoshelevu wa Al-Masihi, ukilinganishwa na utupu wa filosofia ya mwanadamu.Mambo MuhimuMambo yaliyokuwa yakiwasumbua Wakolosai: Mchanganyiko wa elimu ya nyota, uchawi, na mafundisho ya Unostiki ambayo yalisema kwamba Al-Masihi alikuwa sawa na malaika.YaliyomoSalamu, shukrani na maombi (1:1-14)Isa Al-Masihi na waumini (1:15–2:7)Hatari za mafundisho ya uongo (2:8-23)Mafundisho kuhusu maisha ya wafuasi wa Al-Masihi (3:1–4:1)Maagizo zaidi, na mausia ya mwisho (4:2-18).