1 Nyakati Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziJina hili la kitabu “Mambo ya Nyakati” linaweza likafuatiliwa hadi kwa Yerome ambaye alilitumia katika tafsiri ya Kilatini ya Maandiko Matakatifu, yaani “Vulgate.” Jina la kitabu hiki katika Kiyunani, “Mambo Yaliyorukwa,” linaonesha ile hali ya watafsiri wa Maandiko Matakatifu katika “Septuagint” kwamba mambo yaliyomo katika vitabu hivi kimsingi yalikuwa mambo ya nyongeza yaliyokuwa yameachwa na vitabu vya Samweli na Wafalme.Vitabu vya 1 na 2 Mambo ya Nyakati viliandikwa kwa ajili ya watu waliorudi Israeli kutoka utumwani, baada ya kutekwa na kupelekwa Babeli, ili kuwakumbusha kwamba walikuwa wa ukoo wa ufalme wa Daudi, na kwamba wao walikuwa watu wateule wa Mwenyezi Mungu.MwandishiMapokeo ya Kiyahudi husema ni Ezra.KusudiKuunganisha watu wa Mwenyezi Mungu, kufuatilia ukoo wa Daudi, na kufundisha watu sala iliyo ya kweli ambayo ndiyo hitaji kubwa katika maisha ya mtu binafsi na taifa pia.MahaliYerusalemu, na katika Hekalu.TareheKama mwaka wa 430 K.K.Wahusika WakuuDaudi na Sulemani.Wazo KuuKitabu cha 1 Mambo ya Nyakati kinaelezea kwa kifupi historia na koo za Waisraeli tangu Adamu hadi kifo cha Mfalme Sauli. Sehemu ya kitabu iliyobaki inaeleza habari za Mfalme Daudi.Mambo MuhimuKuelezea historia ya vizazi vya Israeli, na habari kumhusu Mfalme Daudi na uhusiano wake na Mwenyezi Mungu, na kuletwa kwa Sanduku la Agano huko Yerusalemu kama chanzo cha sala ya kweli.YaliyomoOrodha ya Vizazi (1:1–9:44)Orodha ya nasaba za mababa wa taifaMakabila ya IsraeliKurudi kutoka utumwani Babeli.Utawala wa Daudi (10:1–29:30)Daudi afanyika mfalme juu ya Israeli yoteDaudi alirudisha Sanduku la Mwenyezi Mungu YerusalemuMajeshi ya Daudi yajinufaishaDaudi aandaa kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu.