2 Wafalme Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziKwa kuwa kitabu cha 1 Wafalme na hiki cha 2 Wafalme ni historia moja inayoendelea, taarifa za msingi za kitabu hiki cha 2 Wafalme ziko katika utangulizi wa 1 Wafalme.MwandishiMwandishi wa kitabu hiki hajulikani, lakini mapokeo ya Kiyahudi yanasema ni nabii Yeremia, au kikundi cha manabii.KusudiKuonesha yale yatakayowapata wale wanaokataa kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa kiongozi wao wa kweli.MahaliKatika nchi ya Israeli.TareheWakati kitabu hiki kiliandikwa haujulikani.Wahusika WakuuIlya, Al-Yasa, mwanamke Mshunami, Naamani, Yezebeli, Yehu, Yoashi, Hezekia, Senakeribu, Isaya, Manase, Yosia, Yehoyakimu, Sedekia, na Nebukadneza.Wazo KuuKuanguka kwa falme zote mbili za Israeli na Yuda kulisababishwa na kutokutii maagizo ya Mwenyezi Mungu, na kuishi maisha ya dhambi. Hali hii iliwapelekea kuwa mateka na kukaa utumwani, nayo miji yao ikaharibiwa; hii ilikuwa hukumu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.Mambo MuhimuKitabu hiki kinaelezea kuhusu majanga mawili yaliyosababisha kuanguka kwa Israeli na Yuda. Janga la kwanza ni kuharibiwa kwa Samaria, mji mkuu wa Israeli, na taifa la Israeli kupelekwa utumwani. Janga la pili ni kuharibiwa kwa Yerusalemu, mji mkuu wa Yuda, na taifa la Yuda kupelekwa utumwani.YaliyomoIlya na Al-Yasa (1:1–8:15)Wafalme wa Israeli na wa Yuda (8:16–17:6)Israeli kutekwa kwenda Ashuru (17:6-41)Wafalme wengine wa Yuda (18:1–24:20)Kuanguka kwa Yerusalemu (25:1-30).