Tito Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziTito, kama vile Timotheo, alikuwa mshirika na rafiki wa karibu wa Paulo katika huduma yake. Alikuwa muumini asiyetahiriwa, mtu wa Mataifa kutoka Antiokia. Alifuatana na Paulo na Barnaba kuhudhuria Baraza la Yerusalemu. Paulo alimwandikia Tito waraka huu muda mfupi tu baada ya kumwachia wajibu wa kuliangalia na kuliimarisha kundi la waumini la Krete. Tito alikuwa na wajibu wa kuwateua wazee wa kundi la waumini, kuwaweka wakfu, na kuwafundisha kushika misingi ya imani ya wafuasi wa Al-Masihi.Waraka huu unaonesha kuwa kundi la waumini la Krete halikuwa na mpangilio mahsusi. Ilimbidi Paulo aeleze kwa kina kuhusu sifa za wazee wa kundi la waumini, na pia kutoa mafundisho kwa waumini. Paulo aligusia matatizo yanayowapata watumishi wa Mwenyezi Mungu, na jinsi yanavyoweza kutatuliwa.MwandishiMtume Paulo.KusudiKumshauri Tito kuhusu wajibu wake wa uangalizi wa makundi ya waumini katika kisiwa cha Krete.MahaliPengine ni Korintho.TareheMnamo 64 B.K.Wahusika WakuuPaulo na Tito.Wazo KuuIngawa katika maisha yetu hapa duniani tumezungukwa na uovu na chuki, hatuna budi maisha yetu kuwa kielelezo jinsi neema ya Mwenyezi Mungu inatupatia ushindi.Mambo MuhimuKuweka mpango na uangalizi wa makundi ya waumini, na jinsi ya kufanya kazi hiyo. Mkazo wa barua hii ni kuhusu kuishi maisha matakatifu katika Al-Masihi katikati ya uovu ulioko duniani. Paulo anarudia mara kwa mara kusisitiza kudumisha matendo mema.YaliyomoSalamu, na wajibu wa Tito huko Krete (1:1-16)Fundisha wote mafundisho manyofu (2:1-15)Maagizo mbalimbali, na maneno ya mwisho (3:1-15).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help