Zaburi 129 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 129Maombi dhidi ya adui za IsraeliWimbo wa kwenda juu.

1Wamenitesa sana tangu ujana wangu;

Israeli na aseme sasa:

2wamenitesa sana tangu ujana wangu,

lakini bado hawajanishinda.

3Wakulima wamelima mgongo wangu,

na kufanya mifereji yao mirefu.

4Lakini Mwenyezi Mungu ni mwenye haki;

amenifungua toka kamba za waovu.

5Wale wote wanaoichukia Sayuni

na warudishwe nyuma kwa aibu.

6Wawe kama majani juu ya paa,

ambayo hunyauka kabla hayajakua;

7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,

wala akusanyaye kujaza mikono yake.

8Wale wapitao karibu na wasiseme,

“Baraka ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako;

tunakubariki katika jina la Mwenyezi Mungu.”

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help