Yeremia 47 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Ujumbe kuhusu Wafilisti

1Hili ndilo neno la Mwenyezi Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaishambulia Gaza:

2Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu:

“Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini,

yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana.

Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyo ndani yake,

miji na wanaoishi ndani yake.

Watu watapiga kelele;

wote wanaoishi katika nchi wataomboleza

3kwa sauti ya kwato za farasi wanaoenda mbio,

kwa sauti ya magari ya vita ya adui,

na mngurumo wa magurudumu yake.

Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao,

mikono yao italegea.

4Kwa maana siku imewadia

kuwaangamiza Wafilisti wote

na kuwakatilia mbali walionusurika wote

ambao wangeweza kusaidia Tiro na Sidoni.

Mwenyezi Mungu anakaribia kuwaangamiza Wafilisti,

mabaki toka pwani za Kaftori.

5Gaza atanyoa kichwa chake katika kuomboleza,

Ashkeloni atanyamazishwa.

Enyi mabaki kwenye tambarare,

mtajikatakata wenyewe hadi lini?

6“Mnalia, ‘Aa, upanga wa Mwenyezi Mungu,

utaendelea hadi lini ndipo upumzike?

Rudi ndani ya ala yako;

acha na utulie.’

7Lakini upanga utatuliaje

wakati Mwenyezi Mungu ameuamuru,

wakati ameuagiza kuishambulia Ashkeloni

pamoja na pwani yake?”

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help