Zaburi 100 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 100Dunia yote yaitwa kumsifu Mwenyezi MunguZaburi ya shukrani.

1Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote.

2Mwabuduni Mwenyezi Mungu kwa furaha;

njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.

3Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu.

Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;

sisi tu watu wake,

kondoo wa malisho yake.

4Ingieni malangoni mwake kwa shukrani

na katika nyua zake kwa kusifu,

mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.

5Kwa maana Mwenyezi Mungu ni mwema

na fadhili zake zadumu milele;

uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help