2 Petro Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziBarua hii inagusia matatizo ambayo Petro aliona yangetukia baada ya kifo chake. Aliwahimiza waumini waendelee kuijua kweli iliyo katika Injili ya Al-Masihi. Kweli hii haikutokana na hadithi za kale, bali ilitokana na mambo waliyoyaona kwa macho. Aliwaonya kuhusu walimu wa uongo ambao wangetukuza mawazo yao wenyewe, badala ya mafundisho ya kweli ya Maandiko Matakatifu. Hatimaye aliwakumbusha waumini kwamba Al-Masihi atakuja siku moja kuangamiza hali ya asili ya ulimwengu huu.MwandishiMtume Petro.KusudiKuwaonya wafuasi wa Al-Masihi kuhusu walimu wa uongo wanaojiingiza ndani ya jumuiya ya waumini, na kuwahimiza kukua katika imani yao na katika kumjua Al-Masihi.MahaliUwezekano mkubwa ni kwamba waraka huu uliandikiwa Rumi.TareheMnamo 67 B.K.Wahusika WakuuPetro na Paulo.Wazo KuuUmuhimu wa kusimama imara katika imani, hata kukiwa na mafundisho mengi ya kupotosha.Mambo MuhimuPetro anashuhudia kwamba Mwenyezi Mungu anataka watu waishi maisha matakatifu kwa ajili ya kukua katika kumcha Al-Masihi. Juu ya yote, anataka wasomaji wake kukaza macho yao katika kuijua kweli ambayo inapatikana tu kwa Isa Al-Masihi, Bwana wetu. Kwa kumjua yeye, waumini wanapokea neema, amani, na mambo yote yapasayo uzima, na utauwa au kumcha Mwenyezi Mungu.YaliyomoNamna ya kukua kiroho (1:1-21)Maonyo kuhusu walimu wa uongo (2:1-22)Siku ya Bwana (3:1-18).