Mathayo Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziMathayo alikuwa mtoza ushuru ambaye Bwana Isa alimwita awe mwanafunzi wake hapo mwanzoni mwa huduma yake ya hadharani. Mathayo alianza kueleza kwa kirefu kuhusu Isa alivyozaliwa na bikira Mariamu, alivyobatizwa, na kujaribiwa nyikani. Isa alihubiri kuhusu ufalme wa Mwenyezi Mungu, ambao ni wa kila mtu anayetaka kupata uzima wa milele. Mtu anaingia katika ufalme huu kwa kutubu dhambi na kumwamini Isa. Mathayo aliyagawa mafundisho ya Isa katika sehemu kuu tano: 1. Maadili, 2. Kueneza Injili, 3. Mifano, 4. Ushirika, na 5. Kuja kwa ufalme wa Mwenyezi Mungu. Sehemu ya mwisho ya Injili ya Mathayo inaeleza kuhusu kufa na kufufuka kwa Isa, na agizo alilolitoa kwa wote wanaomwamini kueneza Injili ulimwenguni kote.MwandishiMathayo aitwaye Lawi.KusudiKumtambulisha Isa kwa Wayahudi kuwa ndiye Masihi, na pia Mfalme wa milele.MahaliPalestina.TareheMnamo 60–65 B.K.Wahusika WakuuIsa na wanafunzi wake, Mariamu, Yahya na wanafunzi wake, viongozi wa dini ya Kiyahudi, na Pilato.Wazo KuuKuthibitisha kwamba Bwana Isa alikamilisha ahadi ambazo Mwenyezi Mungu alitoa katika Maandiko Matakatifu.Mambo MuhimuKitabu hiki kinaelezea matukio manne ya maisha ya Isa ya utotoni. Pia kinaelezea mifano kumi aliyoitoa Isa, na miujiza miwili aliyoifanya. Ina midahalo tisa ambayo Isa alihojiana na baadhi ya watu. Kinamalizia na hisia sita zilizoandamana na kusulubiwa kwake, na maagizo kwa wanafunzi wake kueneza Injili duniani kote.YaliyomoMaisha na huduma ya awali ya Isa (1:1–4:25)Mahubiri ya Mlimani (5:1–7:29)Mafundisho ya mifano na mazungumzo (8:1–18:35)Safari ya kwenda Yerusalemu, na maonyo ya mwisho (19:1–23:39)Unabii kuhusu mambo yajayo (24:1–25:46)Kufa na kufufuka kwa Isa (26:1–28:20).