Zaburi 121 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 121Mwenyezi Mungu mlinzi wetuWimbo wa kwenda juu.

1Nayainua macho yangu natazama milima:

msaada wangu utatoka wapi?

2Msaada wangu hutoka kwa Mwenyezi Mungu,

Muumba wa mbingu na dunia.

3Hatauacha mguu wako uteleze,

yeye akulindaye hatasinzia,

4hakika, yeye alindaye Israeli

hatasinzia wala hatalala usingizi.

5Mwenyezi Mungu anakulinda,

Mwenyezi Mungu ni uvuli wako mkono wako wa kuume,

6jua halitakudhuru mchana,

wala mwezi wakati wa usiku.

7Mwenyezi Mungu atakukinga na madhara yote,

atayalinda maisha yako,

8Mwenyezi Mungu atakulinda unapoingia na unapotoka,

tangu sasa na hata milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help