Filemoni Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziWaraka huu mfupi umeainishwa na nyaraka za Waefeso, Wakolosai na Wafilipi kama mojawapo wa nyaraka Paulo alizoandika akiwa gerezani. Aliandikia Filemoni na Afia, mwanamke mfuasi wa Al-Masihi (ambaye huenda alikuwa mkewe Filemoni), na Arkipo, na kundi la waumini lililokuwa likikusanyika nyumbani mwa Filemoni.Onesimo alikuwa mtumwa aliyetoroka kutoka kwa Filemoni huko Kolosai akaenda Rumi, ambako aliokoka. Onesimo, kama mtumwa, alikuwa mali ya Filemoni kisheria.MwandishiMtume Paulo.KusudiKumhimiza Filemoni amsamehe Onesimo, mtumwa aliyemtoroka, na amkubali kama ndugu mfuasi wa Al-Masihi katika imani.MahaliRumi.TareheMnamo 60 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Filemoni, na Onesimo.Wazo KuuPaulo alimwandikia Filemoni kumshawishi amkubali Onesimo kurudi kwake, na amsamehe aliyomkosea.Mambo MuhimuBarua hii ni kielelezo cha ukarimu wa wafuasi wa Al-Masihi. Paulo alishukuru kwa moyo wa ukarimu ambao tayari Filemoni alikuwa ameonesha kwa wafuasi wa Al-Masihi wenzake. Paulo alikuwa na uwezo wa kumwamuru Filemoni, lakini alimwomba Filemoni ampokee Onesimo kwa upendo.YaliyomoSalamu (1-3)Shukrani na maombi (4-7)Paulo anamtetea Onesimo (8-22)Salamu za mwisho (23-25).