Zaburi 36 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 36Uovu wa mwanadamuKwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi mtumishi wa Mwenyezi Mungu.

1Kuna neno moyoni mwangu

kutoka kwa Mungu

kuhusu hali ya dhambi ya mwovu.

Hakuna hofu ya Mungu

mbele ya macho yake.

2Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno

hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake.

3Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu,

ameacha kuwa mwenye hekima au kutenda mema.

4Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya,

hujitia katika njia ya dhambi

na hakatai lililo baya.

5Upendo wako, Ee Mwenyezi Mungu, unafika hadi mbinguni,

uaminifu wako hadi kwenye anga.

6Haki yako ni kama milima mikubwa,

hukumu zako ni kama kilindi kikuu.

Ee Mwenyezi Mungu, wewe huwahifadhi

mwanadamu na mnyama.

7Upendo wako usiokoma

ni wa thamani mno!

Watu wakuu na wadogo

hujificha uvulini wa mabawa yako.

8Wanajifurahisha katika wingi ulio nyumbani mwako,

nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako.

9Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima,

katika nuru yako twaona nuru.

10Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe,

haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo.

11Mguu wa mwenye kiburi usije dhidi yangu,

wala mkono wa mwovu usinifukuze.

12Tazama jinsi watenda maovu walivyoanguka:

wametupwa chini, hawawezi kuinuka!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help