Zaburi 8 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 8Utukufu wa Mwenyezi Mungu na heshima ya mwanadamuKwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Daudi.

1Ee Mwenyezi Mungu, Bwana wetu,

tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!

Umeuweka utukufu wako

juu ya mbingu.

2Midomoni mwa watoto wachanga na wanaonyonya

umeamuru sifa,

kwa sababu ya watesi wako,

kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi.

3Nikiziangalia mbingu zako,

kazi ya vidole vyako,

mwezi na nyota,

ulizoziratibisha,

4mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria,

binadamu ni nani hata unamjali?

5Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni,

ukamvika taji la utukufu na heshima.

6Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako;

umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.

7Mifugo na makundi yote pia,

naam, na wanyama wa kondeni,

8ndege wa angani na samaki wa baharini,

naam, kila kinachoogelea katika njia za bahari.

9Ee Mwenyezi Mungu, Bwana wetu,

tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help