Ayubu 25 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Bildadi anasema: Mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mwenyezi Mungu?

1Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu:

2“Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu;

yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.

3Je, majeshi yake yaweza kuhesabika?

Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?

4Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?

Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?

5Ikiwa hata mwezi sio mwangavu

nazo nyota si safi machoni pake,

6sembuse mtu ambaye ni funza:

mwanadamu ambaye ni buu tu!”

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help