Mika Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziJina “Mika” maana yake ni “Ni nani aliye kama Mwenyezi Mungu”. Mika alikuwa mkaazi wa mji wa Moresheth-Gathi kusini mwa Yuda, na aliishi wakati mmoja na Isaya na Hosea. Aliona Waashuru wakiendelea kustawi wakati Israeli ilikuwa ikididimia hadi ikawa jimbo la Ashuru baada ya kuanguka kwa Israeli mnamo 722 K.K. Yuda mara kwa mara ilipata vitisho kutoka kwa wafalme wa Ashuru waliofanikiwa. Mika alionya kuhusu hukumu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya falme zote mbili za Yuda na Israeli.Hali kadhalika, alitabiri kuangamizwa kwa falme hizo kwa sababu ya uovu wa watawala, manabii wa uongo, makuhani waovu, wafanyabiashara wasio waaminifu, na mahakimu waliouza haki kwa rushwa. Kimsingi, Mika alitangaza hukumu kwa Yuda na Israeli kwa watawala, viongozi wa dini, wasimamizi wa haki, na matajiri hawakuwa na uchaji wala hofu ya Mwenyezi Mungu katika kutimiza wajibu wao. Mbali na kutangaza hukumu dhidi ya waovu, pia Mika alitoa ujumbe wa matumaini. Alitangaza ahadi ya kufanywa upya kwa Sayuni na utawala wa amani kwa waliomwamini na kumtumaini Mwenyezi Mungu. Alihubiri kwamba Sayuni mpya itakuwa kitovu cha utawala wa ulimwengu wote, mahali ambapo haki na amani halisi vitatamalaki. Sayuni mpya ilihusishwa kuwepo na “Mtawala katika Israeli” yaani Masihi, ambaye angezaliwa Bethlehemu na kuanzisha utawala wake ambao utadumu milele.MwandishiMika.KusudiKuwaonya mataifa ya Yuda na Israeli juu ya hukumu ya Mwenyezi Mungu na kutangaza wokovu kwa wote watakaotubu na kuamini katika Masihi atakayezaliwa Bethlehemu.MahaliSamaria na Yerusalemu.TareheMnamo 742–687 K.K.Wahusika WakuuWatu wa Samaria na Yerusalemu.Wazo KuuHukumu na wokovu wa Masihi.Mambo MuhimuHuu ni mfano mzuri wa ushairi wa Kiebrania. Ziko sehemu tatu, kila moja ikianza na “Sikia” au “Sikiliza” (1:2; 3:1; 6:1) na kufunga na ahadi.YaliyomoHukumu dhidi ya Samaria na Yerusalemu (1:1-16)Mipango ya mwanadamu na mipango ya Mwenyezi Mungu (2:1–3:12)Urejesho wa Mwenyezi Mungu (4:1–5:15)Hukumu na huruma (6:1–7:20).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help