Malaki Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziMaana ya jina Malaki ni “Mjumbe Wangu” au “Mjumbe wa Mwenyezi Mungu”. Malaki aliishi baada ya Hekalu la pili kujengwa. Maisha ya uchaji wa Mwenyezi Mungu ya Wayahudi yalikuwa mabaya: Walikuwa wamekengeuka, wakawaoa wanawake wa mataifa mengine, na wakaacha kutoa zaka na dhabihu kwa Mwenyezi Mungu. Habari hizi zinafanana sana na mwisho wa kitabu cha Nehemia, ambaye kuna uwezekano mkubwa aliishi wakati mmoja na Malaki.MwandishiMalaki.KusudiKuwahimiza watu wafanye mabadiliko thabiti ya kimsingi katika maisha yao kwa kuziacha dhambi zao ili kurejesha uhusiano wao na Mwenyezi Mungu, na kuwakumbusha kuhusu upendo wa Mwenyezi Mungu.MahaliYerusalemu na Hekaluni.TareheMnamo 430 K.K.Wahusika WakuuMalaki, makuhani, na watu wa Yuda.Wazo KuuUpendo wa Mwenyezi Mungu hauna kikomo wala mipaka.Mambo MuhimuKitabu hiki kinaonesha kuwa Hekalu lilijengwa tena, na dhabihu na sikukuu zikarudishwa. Ufahamu wa jumla wa Torati ulirudishwa tena na Ezra, na kurudi kwao nyuma kimaadili kulikofuatia kulitokea zaidi miongoni mwa makuhani.YaliyomoUpendo wa Mwenyezi Mungu kwa Israeli (1:1-5)Israeli wamtukana Mwenyezi Mungu (1:6–2:16)Hukumu ya Mwenyezi Mungu na ahadi yake (2:17–4:6).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help