1Baada ya Abimeleki, Tola mwana wa Pua mwana wa Dodo, mtu wa Isakari, aliyeishi huko Shamiri, katika nchi ya vilima ya Efraimu, akainuka kuokoa Israeli.
2Akawa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini na tatu. Ndipo akafa, naye akazikwa huko Shamiri.
Yairi3Baada yake akafuatiwa na Yairi, Mgileadi, aliyekuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini na mbili.
4Alikuwa na wana thelathini waliopanda punda thelathini. Nao walikuwa na miji thelathini huko Gileadi, inayoitwa Hawoth-Yairi hadi leo.
5Yairi akafa, naye akazikwa huko Kamoni.
Yefta6Tena Waisraeli wakatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu. Wakaabudu Mabaali na Maashtorethi, na miungu ya Aramu, miungu ya Sidoni, miungu ya Moabu, miungu ya Waamoni, na miungu ya Wafilisti. Na kwa kuwa Waisraeli walimwacha Mwenyezi Mungu wala hawakuendelea kumtumikia,
7hivyo hasira ya Mwenyezi Mungu ikawaka dhidi ya Waisraeli. Naye akawatia mikononi mwa Wafilisti na Waamoni,
8ambao waliowaonea na kuwatesa mwaka huo. Kwa miaka kumi na nane wakawatesa Waisraeli wote upande wa mashariki mwa Mto Yordani huko Gileadi, katika nchi ya Waamori.
9Waamoni nao wakavuka Yordani ili kupigana na Yuda, Benyamini na nyumba ya Efraimu, nayo nyumba ya Israeli ikawa katika taabu kubwa.
10Ndipo Waisraeli wakamlilia Mwenyezi Mungu wakasema, “Tumetenda dhambi dhidi yako, kumwacha Mungu wetu na kutumikia Mabaali.”
11Mwenyezi Mungu akawaambia, “Wamisri, Waamori, Waamoni, Wafilisti,
12Wasidoni, Waamaleki na Wamaoni walipowadhulumu ninyi, nanyi mkanililia na kuomba msaada, je, sikuwaokoa mikononi mwao?
13Lakini ninyi mmeniacha na kuitumikia miungu mingine, kwa hiyo sitawaokoa tena.
14Nendeni mkaililie ile miungu mlioichagua. Hiyo miungu na iwaokoe mnapokuwa katika taabu!”
15Lakini Waisraeli wakamwambia Mwenyezi Mungu, “Tumetenda dhambi. Ututendee lile unaloona kuwa jema kwako, lakini twakusihi utuokoe sasa.”
16Nao wakaiondoa hiyo miungu migeni kati yao nao wakamtumikia Mwenyezi Mungu. Naye akahuzunika kwa sababu ya taabu ya Israeli.
17Waamoni walipoitwa vitani na kupiga kambi kule Gileadi, Waisraeli walikusanyika na kupiga kambi huko Mispa.
18Viongozi wa watu wa Gileadi wakaambiana wao kwa wao, “Yeyote atakayeanzisha mashambulizi dhidi ya Waamoni atakuwa kiongozi wa wote wanaoishi Gileadi.”
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.