1Heri mtu yule ambaye haendi
katika shauri la watu waovu,
wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,
au kuketi katika baraza la wenye mizaha.
2Bali huifurahia Torati ya Mwenyezi Mungu,
naye huitafakari hiyo Torati usiku na mchana.
3Mtu huyo ni kama mti uliopandwa
kando ya vijito vya maji,
ambao huzaa matunda kwa majira yake
na majani yake hayanyauki.
Lolote afanyalo hufanikiwa.
Huzuni ya waovu4Sivyo walivyo waovu!
Wao ni kama makapi
yanayopeperushwa na upepo.
5Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,
wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
6Kwa maana Mwenyezi Mungu huziangalia njia za mwenye haki,
bali njia za waovu zitaangamia.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.