Zaburi 130 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 130Kumngojea Mwenyezi MunguWimbo wa kwenda juu.

1Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Mwenyezi Mungu.

2Ee Bwana, sikia sauti yangu.

Masikio yako na yawe masikivu

kwa kilio changu unihurumie.

3Kama wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ungeweka kumbukumbu ya dhambi,

Ee Bwana, ni nani angeweza kusimama?

4Lakini kwako kuna msamaha,

kwa hiyo wewe unaogopwa.

5Namngojea Mwenyezi Mungu, nafsi yangu inangojea,

katika neno lake naweka tumaini langu.

6Nafsi yangu inamngojea Bwana

kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,

naam, kuliko walinzi

waingojeavyo asubuhi.

7Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungu,

maana kwa Mwenyezi Mungu kuna upendo usiokoma,

na kwake kuna ukombozi kamili.

8Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli

kutoka dhambi zao zote.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help