1Basi viongozi wa watu walikaa Yerusalemu, nao watu wale wengine walipiga kura ili kuleta mtu mmoja kati ya watu kumi aje kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, nao wengine tisa waliobaki wakae katika miji yao wenyewe.
2Watu waliwasifu wale wote waliojitolea kuishi Yerusalemu.
3Hawa ndio viongozi wa majimbo waliokuja kuishi Yerusalemu (baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi, watumishi wa Hekalu, na wazao wa watumishi wa Sulemani waliendelea kuishi katika miji ya Yuda, kila mmoja katika milki yake mwenyewe katika miji mbalimbali,
4ambapo watu wengine kutoka Yuda na Benyamini waliishi Yerusalemu).
Kutoka wazao wa Yuda:
Athaya mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli, mzao wa Peresi.
5Naye Maaseya mwana wa Baruku, mwana wa Kolhoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zekaria, mzao wa Mshiloni.
6Wazao wa Peresi walioishi Yerusalemu walikuwa mia nne sitini na nane (468), wanaume wenye uwezo.
7Kutoka wazao wa Benyamini:
Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Maaseya, mwana wa Ithieli, mwana wa Yeshaya
8na wafuasi wake, Gabai na Salai: wanaume mia tisa ishirini na nane (928).
9Yoeli mwana wa Zikri alikuwa afisa wao mkuu, naye Yuda mwana wa Hasenua alikuwa msimamizi juu ya Mtaa wa Pili katika mji.
10Kutoka makuhani:
Yedaya; mwana wa Yoyaribu; Yakini;
11Seraya mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, msimamizi wa nyumba ya Mungu,
12pamoja na wenzao waliofanya kazi hekaluni: wanaume mia nane ishirini na wawili (822).
Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amzi, mwana wa Zekaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya,
13na wenzao, waliokuwa viongozi wa jamaa: wanaume mia mbili arobaini na wawili (242).
Amashisai mwana wa Azareli, mwana wa Azai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri,
14na wenzao waliokuwa wanaume wenye uwezo: mia moja ishirini na nane (128).
Afisa wao mkuu alikuwa Zabdieli mwana wa Hagedolimu.
15Kutoka Walawi:
Shemaya mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, mwana wa Buni;
16Shabethai na Yozabadi, viongozi wawili wa Walawi, ambao walisimamia kazi za nje za nyumba ya Mungu;
17Matania mwana wa Mika, mwana wa Zabdi, mwana wa Asafu, kiongozi aliyeongoza kutoa shukrani na maombi;
Bakbukia aliyekuwa msaidizi wake kati ya wenzake;
na Abda mwana wa Shamua, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.
18Jumla ya Walawi waliokaa katika mji mtakatifu walikuwa wanaume mia mbili themanini na wanne (284).
19Mabawabu:
Akubu, Talmoni na wenzao, waliolinda malango: wanaume mia moja sabini na wawili (172).
20Waisraeli waliosalia, pamoja na makuhani na Walawi, walikuwa katika miji yote ya Yuda, kila mmoja katika urithi wa baba yake.
21Watumishi wa Hekalu waliishi katika kilima cha Ofeli. Siha na Gishpa walikuwa wasimamizi wao.
22Afisa mkuu wa Walawi huko Yerusalemu alikuwa Uzi mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika. Uzi alikuwa mmoja wa wazao wa Asafu, waliokuwa waimbaji wenye kuwajibika kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu.
23Waimbaji walikuwa chini ya amri za mfalme, ambazo pia ziliratibu shughuli zao za kila siku.
24Pethahia mwana wa Meshezabeli, mmoja wa wazao wa Zera mwana wa Yuda, alikuwa mwakilishi wa mfalme katika mambo yote kuhusu mahusiano na watu.
25Kuhusu vijiji na mashamba yake, baadhi ya watu wa Yuda waliishi Kiriath-Arba na makazi yaliyouzunguka, katika Diboni na makazi yake, katika Yekabzeeli na vijiji vyake,
26katika Yeshua, katika Molada, katika Beth-Peleti,
27katika Hasar-Shuali, katika Beer-Sheba na makazi yake,
28katika Siklagi, katika Mekona na makazi yake,
29katika En-Rimoni, katika Sora, katika Yarmuthi,
30Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, katika Lakishi na mashamba yake, na katika Azeka na makazi yake. Hivyo walikuwa wakiishi kuanzia Beer-Sheba hadi Bonde la Hinomu.
31Wazao wa Wabenyamini kutoka Geba waliishi Mikmashi, Aiya, Betheli na makazi yake,
32katika Anathothi, Nobu na Anania,
33katika Hazori, Rama na Gitaimu,
34katika Hadidi, Seboimu na Nebalati,
35katika Lodi na Ono, na katika Bonde la Mafundi.
36Baadhi ya makundi ya Walawi wa Yuda waliishi huko Benyamini.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.