Zaburi 82 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 82Maombi kwa ajili ya kutaka hakiZaburi ya Asafu.

1Mungu anaongoza kusanyiko kuu,

anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:

2“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki

na kuonesha upendeleo kwa waovu?

3Teteeni wanyonge na yatima,

tunzeni haki za maskini na waliodhulumiwa.

4Mwokoeni mnyonge na mhitaji,

wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.

5“Hawajui lolote, hawaelewi lolote.

Wanatembea gizani;

misingi yote ya dunia imetikisika.

6“Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”;

ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’

7Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida;

mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”

8Ee Mungu, inuka uihukumu nchi,

kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help