Zaburi 16 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 16Sala ya matumainiUtenzi wa Daudi.

1Ee Mungu, uniweke salama,

kwa maana kwako nimekimbilia.

2Nilimwambia Mwenyezi Mungu, “Wewe ndiwe Bwana wangu;

pasipo wewe sina jambo jema.”

3Kuhusu watakatifu walio duniani,

hao ndio wenye fahari,

na ninapendezwa nao.

4Huzuni itaongezeka kwa wale

wanaokimbilia miungu mingine.

Sitazimimina sadaka za damu kwa miungu kama hiyo,

au kutaja majina yao mdomoni mwangu.

5Mwenyezi Mungu umeniwekea fungu langu na kikombe changu;

umeyafanya mambo yangu yote yawe salama.

6Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri,

hakika nimepata urithi mzuri.

7Nitamsifu Mwenyezi Mungu ambaye hunishauri,

hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.

8Nimemweka Mwenyezi Mungu mbele yangu daima.

Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,

sitatikisika.

9Kwa hiyo moyo wangu unafurahia,

na ulimi wangu unashangilia;

mwili wangu nao

utapumzika salama,

10kwa maana hutaniacha Kuzimu,

wala hutamwacha Mtakatifu Wako

kuona uharibifu.

11Umenijulisha njia ya uzima;

utanijaza na furaha mbele zako,

pamoja na furaha ya milele

katika mkono wako wa kuume.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help