1Mpeni Mwenyezi Mungu, enyi mashujaa,
mpeni Mwenyezi Mungu utukufu na nguvu.
2Mpeni Mwenyezi Mungu utukufu unaostahili jina lake;
mwabuduni Mwenyezi Mungu katika uzuri wa utakatifu wake.
3Sauti ya Mwenyezi Mungu iko juu ya maji;
Mungu wa utukufu hupiga radi,
Mwenyezi Mungu hupiga radi juu ya maji makuu.
4Sauti ya Mwenyezi Mungu ina nguvu;
sauti ya Mwenyezi Mungu ni tukufu.
5Sauti ya Mwenyezi Mungu huvunja mierezi;
Mwenyezi Mungu huvunja vipande vipande
mierezi ya Lebanoni.
6Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,
Sirioni urukaruke kama mwana nyati.
7Sauti ya Mwenyezi Mungu hupiga
kwa miali ya radi.
8Sauti ya Mwenyezi Mungu hutikisa jangwa;
Mwenyezi Mungu hutikisa Jangwa la Kadeshi.
9Sauti ya Mwenyezi Mungu huzalisha ayala,
na huuacha msitu wazi.
Hekaluni mwake wote wasema,
“Utukufu!”
10Mwenyezi Mungu huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika;
Mwenyezi Mungu ametawazwa kuwa Mfalme milele.
11Mwenyezi Mungu huwapa watu wake nguvu;
Mwenyezi Mungu huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.