Yohana Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziMiongoni mwa Injili zote nne, Injili ya Yohana ni ya kipekee. Ingawa kwa ujumla inaonesha maisha ya Isa na huduma yake, Injili hii haina mifano. Injili ya Yohana inaelezea miujiza saba; kuna miwili iliyonakiliwa katika Injili zile zingine, na miujiza mitano ambayo Yohana peke yake aliielezea.Yohana anaandika jinsi Isa anavyojidhihirisha kuwa ni Mwenyezi Mungu kwa semi saba za “Mimi Ndiye”. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyojidhihirisha kwa Waisraeli huko Misri. Kwa hiyo, ni wazi kwamba Isa ni Yehova.MwandishiYohana mwana wa Zebedayo, nduguye Yakobo.Kusudi“Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Isa ndiye Al-Masihi, Mwana wa Mwenyezi Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake” (20:31).MahaliUwezekano mkubwa ni kwamba Injili hii iliandikiwa Efeso.TareheMnamo 85–90 B.K.Wahusika WakuuIsa, mama yake, na wanafunzi wake Isa; Yahya na wanafunzi wake; Mariamu, Martha na Lazaro; Pilato, wakuu wa dini ya Kiyahudi, na Mariamu Magdalene.Wazo KuuInjili ya Yohana inatilia mkazo zaidi Uungu wa Al-Masihi. Pia inatueleza kwa undani zaidi ishara ambazo Injili zingine zinaziita miujiza, ili msomaji aweze kuamini kwamba Isa ndiye Al-Masihi, Mwana wa Mwenyezi Mungu, na kwamba mtu anaweza kupata uzima wa milele tu kwa kumwamini Isa.Mambo MuhimuKatika Injili hii, tunapata habari kuhusu baadhi ya miujiza ya Isa, na mafundisho yake ambayo hayakutajwa katika Injili zingine. Sehemu ya sura 14–17 inaeleza kwa kina mafundisho ambayo Isa aliwapa wanafunzi wake kabla ya kifo chake. Sehemu ya mwisho inafafanua jinsi Isa alivyojidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwake.YaliyomoNeno alifanyika mwili (1:1-18)Huduma ya Isa kabla ya kurudi Galilaya (1:19–4:54)Huduma ya Isa huko Galilaya, na upinzani uliomkabili huko Yerusalemu (5:1–10:42)Isa amfufua Lazaro (11:1-57)Isa akamilisha huduma yake (12:1–13:30)Mafundisho ya mwisho ya Bwana Isa (13:31–17:26)Kufa na kufufuka kwa Isa (18:1–20:10)Isa aonekana baada ya kufufuka (20:11–21:25).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help