Zaburi 21 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 21Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya ushindiKwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1Ee Mwenyezi Mungu, mfalme huzifurahia nguvu zako.

Tazama jinsi furaha yake ilivyo kuu

kwa ushindi unaompa!

2Umempa haja ya moyo wake

na hukumzuilia maombi ya midomo yake.

3Ulimkaribisha kwa baraka tele

na kumvika taji la dhahabu safi kichwani pake.

4Alikuomba maisha, nawe ukampa,

wingi wa siku milele na milele.

5Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa,

umeweka juu yake fahari na utukufu.

6Hakika umempa baraka za milele,

umemfanya awe na furaha

kwa shangwe ya uwepo wako.

7Kwa kuwa mfalme anamtumaini Mwenyezi Mungu;

kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.

8Mkono wako utawashika adui zako wote,

mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.

9Wakati utajitokeza,

utawafanya kama tanuru la moto.

Katika ghadhabu yake Mwenyezi Mungu atawameza,

moto wake utawateketeza.

10Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani,

uzao wao kutoka wanadamu.

11Ingawa watapanga mabaya dhidi yako

na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa,

12kwa kuwa utawafanya wakimbie

utakapowalenga usoni pao

kwa mshale kutoka upinde wako.

13Ee Mwenyezi Mungu, utukuzwe katika nguvu zako,

tutaimba na kusifu nguvu zako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help