Mhubiri Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziNeno “Mhubiri” linatokana na neno la Kiebrania “Qoheleth” ambalo linamaanisha “Anayehutubia kusanyiko la watu”, na linatafsiriwa kama “Mwalimu” katika “Septuaginta”. Mara kwa mara mwandishi wa kitabu hiki anajitambulisha mwenyewe kuwa “Mhubiri”. Neno hili limetumiwa mara saba katika kitabu hiki. Hivyo, ilionekana inafaa kutumia neno hili kukitambulisha kitabu hiki.MwandishiInadhaniwa kuwa ni Sulemani.KusudiKuchunguza kwa kina maana ya maisha kwa ujumla, na kuonesha kuwa maisha hayana maana, yaani ni ubatili, kama hakuna kumcha Mwenyezi Mungu kikamilifu.MahaliYerusalemu.TareheInadhaniwa kuwa mwaka 935 K.K., mwishoni mwa maisha ya Sulemani.Wahusika WakuuSulemani.Wazo KuuIli kuelewa maisha na kufanya uamuzi ulio sawa, binadamu anahitaji hekima ambayo inapatikana kwa kumjua Mwenyezi Mungu pekee.Mambo MuhimuKuonesha jinsi kufuata starehe maishani kunaweza kuleta udanganyifu wa dhambi na kutukosesha utoshelevu na furaha. Chanzo cha furaha, mafanikio na utoshelevu ni kumcha Mwenyezi Mungu na kuzishika amri zake. Kama mtu yeyote ataishi na Mwenyezi Mungu daima, basi kumtii Mwenyezi Mungu ndio njia pekee ya kufanikiwa katika maisha ya hapa duniani.YaliyomoMaisha ni ubatili mtupu (1:1-11)Kikomo cha hekima (1:12–2:26)Kila jambo lina wakati wake (3:1-22)Ugumu wa maisha na kumcha Mwenyezi Mungu (4:1–6:12)Hekima na kutosheka (7:1–8:17)Maisha ni lazima yatawaliwe na hekima (9:1–11:6)Hekima ya kweli ni kumcha Mwenyezi Mungu (11:7–12:14).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help